Franklin Emoubor, raia wa Nigerian
ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamuziki nyota wa kike nchini Uganda
Desire Luzinda amekamatwa.
Waziri wa Maadili wa Uganda
Mchungaji Simon Lokodo, amesema kuwa Mnaigeria huyo amekamatwa na
kikosi cha polisi cha kimataifa cha Interpol.
Hata hivyo waziri huyo hakueleza
iwapo Emoubor anayedaiwa kusambaza mtandaoni picha za utupu za
Desire, amekamatwa akiwa wapi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni