Mkutano wa siku tatu unaojadili
namna ya kukabiliana na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na vikundi
vyenye kufuata itikati kali, umeanza nchini Marekani.
Wawakilishi kutoka pande zote za
dunia wanahudhuria mkutano huo, ambao umeitishwa kufuatia matukio ya
mauaji yaliyotokea Denmark, Ufaransa na Australia.
Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden
amesema ni muhimu kushirikiana na wahamiaji ambao wanaweza
kushawishika kujihusisha na makundi hayo kutokana na kujihisi
wametengwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni