Walinzi wa Pwani ya Italia
wamewaokoa wahamiaji haramu zaidi ya 2,000 katika operesheni kubwa
iliyofanyika kwenye eneo la Pwani ya Libya.
Maafisa wa Italia wamesema wakati wa
zoezi hilo timu ya waokoaji ilitishiwa kwa silaka ya AK 45 na mtu
aliyekuwa akiwakaribia akiwa kwenye boti ya mwendo kasi akitokea
Libya.
Wiki iliyopita wahamiaji haramu
wapatao 300 walikufa maji katika bahari ya Mediterranean, wakati
wakielekea nchi za Ulaya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni