Mwanamke aliyejitoa mhanga kwa
mlipuko wa bomu ameuwa watu wapatao saba katika kituo cha basi chenye
watu wengi kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Polisi wamesema zaidi ya watu 30
wengine wamejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea kwenye mji wa
Damaturu ambao ni mji Mkuu wa Jimbo la Yobe.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika na
shambulio hilo, lakini kundi la jihadi la Boko Haram katika siku za
nyuma lilishafanya mashambulizi katika mji huo.
Siku ya jumapili wapiganaji wa kundi
la Boko Haram walijaribu kuutwaa mji wa mkuu wa jimbo la Gombe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni