.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Februari 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AREJEA NCHINI AKITOKEA QATAR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Marubani wa Ndege ya Serekali baada ya kuwasili uwanja wa Kamataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Qatar alikokuwa na ziara ya Kiserikali Nchini humo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akivishwa shada la mauwa na Vijana walioandaliwa wakati wa mapokezi yake baada ya kumaliza ziara yake Nchi Qatar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui, alipowasili uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Viongozi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
  Maalim akisalimia na Wananchi waliofika kumpokea akitokea ziarani Nchi Qatar.
Maalim Seif akiangaliwa wanafunzi wa Madrasa wakipiga Dufu wakati wa mapokezi yake Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Waandishi wa habari mbalimbali waliofika uwanja wa ndege wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumzia mafanikio ya ziara yake Nchi Qatar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake Nchini Qatar hivi karibuni na kuzungumzia mafanikio ya ziara hiyo kwa waandishi waliofika katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume. mkutano huo umehudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar.
Mwandishi wa ZBC Ndg,Maulid Kipevu akiuliza swali wakati wa mkutano na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
Mwandishi wa Redio Adhana Ndg Said Mussa alipata fursa ya kuuliza swli katika mkutano huo.
Maalim Seif akijibu maswala alioulizwa na waandishi wakati wa mkutano na waandishi alipowasili Zanzibar akitokea ziarani Nchini Qatar.

Waheshimiwa wakimsikiliza Maalim Seif alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.katika ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

                      Waandishi wakimsikiliza Maalim Seif akijibu maswala ya waandishi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni