Mmoja wa wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la
uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy pamoja na
mwanae wakijaza fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es
Salaam.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu maarufu
duniani ya mpira wa miguu ya Real Madrid ya Hispania, leo imeendelea na
zoezi lake la usajili wa vijana walio na umri wa chini ya miaka 14
watakaofanyiwa majaribio kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha
NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY katika uwanja wa Karume mjini Dar es
Salaam, huku idadi ya vijana wanaojisajili ikiongezeka.
Mchakato
huo wa usajili ulianza Oktoba 14 lakini leo idadi ya vijana
wanaojitokeza ikiongezeka kwa kasi ambapo jumla ya vijana 257
wamejitokeza kuandikiswa katika viwanja vya karume jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
zoezi hilo kwa wanahabari katika viwanja vya Karume, Kaimu Meneja
Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Salim Khalfan Kimaro
wa NSSF, alisema uandikishaji wa vijana katika zoezi hilo leo
umeongezeka kutokana na idadi kubwa kujitokeza kuandikishwa.
Akitoa
ufafanuzi zaidi Kimaro alisema watoto walengwa ni wale waliozaliwa
kuanzia Januari, 2001 hadi Disemba, 2003 na ili mtoto aandikishwe
anatakiwa kuambatana na mzazi wake au mlezi anayetambulika kisheria na
aje na nyaraka za uthibitisho wake kuwa ni mlezi halali kwa kuonesha
vithibitisho vya kisheria.
“…Kwa mtoto husika,
aje na cheti halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha ndogo
(passport size) zenye rangi ya bluu. Zoezi hili litaendelea tena wiki
ijayo tarehe 21 na 22 Februari ambapo baada ya hapo michezo ya majaribio
itaanza wiki zinazofuatia,” alisema Khalfan Kimaro.
Aidha
aliongeza kuwa watoto 30 watakao fuzu kuingia katika kituo cha mafunzo
wataandaliwa mazingira kuhakikisha wanaendelea kupata elimu bila kikwazo
chochote. Alisema Shirika la NSSF linatoa wito kwa wazazi na walezi
kujitokeza kuwaleta watoto wao kujiandikisha ili kuendeleza vipaji vyao
kwa fursa iliyotolewa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni