Watazamaji wa televisheni Jijini
Nairobi nchini Kenya wamejikuta wakikabiliana na runinga
zisizoonyesha kitu hapo jana baada ya mamlaka ya mawasiliano kuvamia
vituo vinne vya televisheni na kuzima matangazo yake.
Wakiambatana na ulinzi mkali wa
polisi, maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya waliangia kwa nguvu
kwenye eneo la Limuru lenye mitambo ya kurusha matangazo ya analogi
ya vituo vya NTV, QTV, Citizen TV na KTN na kuzima mitambo inayotoa
matangazo kwa eneo la Nairobi.
Uamuzi huo wa Mamalaka ya
Mawasiliano Kenya, unafuatia maamuzi ya mahakama yaliyotolewa Ijumaa,
ambayo yamesisitiza Desemba 31, 2014 ndio ulikuwa mwisho wa
televisheni zote Kenya kurusha matangazo yao Jijini Nairobi kwa njia
ya analogi, na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na vituo vitatu.
Kuzimwa matangazo ya vituo hivyo
vinne vya televisheni kumewanyima asilimia 90 ya wananchi wa Kenya
wanaotegemea matangazo ya vituo hivyo kuangalia habari pamoja na
vipindi vingine, na pia kumevunja haki ya kikatiba ya uhuru wa kupata
habari bila malipo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni