Misri imetoa wito wa kutaka kuwepo
ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na wapiganaji
wa kundi la dola ya Kiislam IS nchini Libya.
Rais Abdel Fattah al-Sisi amesema
kinachofanyika nchini Libya ni tisho kwa amani ya dunia na usalama.
Kauli ya rais al-Sis imekuja wakati
ndege za kivita za Misri zikishambulia maeneo ya wapiganaji wa IS
katika kujibu mapigo kwa tukio la kuuwawa kwa kuchinjwa Wamisri 21
wakristo na wapiganaji wa IS.
Nchi ya Libya imekuwa katika
machafuko tangu mwaka 2011, huku kukiwa na vikundi vya wapiganaji
vipatavyo 1,400 vikipigana kushika utawala wa maeneo, licha ya kuwa
pia na serikali mbili kinzani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni