Mwanamke mmoja mwenye bahati
amenusurika kufa maji baada ya kuokolewa na polisi kufuatia gari lake
aina ya BMW kuzama haraka baada ya kutumbukia majini kwenye bandari
ya Waitemata huko Auckland nchini New Zealand.
Mwanamke huyo aliyekuwa amejawa na
hofu alikuwa amekimbilia kwenye kioo cha nyuma baada ya sehemu ya
gari lake la mbele kuzama haraka baada ya gari lake kuzama haraka
baada ya kutumbukia.
Polisi walijaribu kuvunja kioo cha
nyuma cha gari kwa kutumia virungu vyao lakini walishindwa na ndipo
polisi mmoja alipookota jiwe na kutumia kuvunja kioo hicho na
kufanikiwa kukivunja na kumtoa kabla ya mwanamke huyo hajaishiwa na
pumzi.
Polisi akitumia jiwe kuvunja kioo cha gari lililokuwa likizama
Hatimae mwanamke huyo akiokolewa kutoka kwenye gari lake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni