Makumi ya maelfu ya watu
wamekusanyika katika miji kadhaa nchini Denmark kuwakumbuka wahanga
wa matukio ya mashambulizi ya silaha yaliyotokea katika Jiji la
Copenhagen.
Watu waliobeba mishumaa na tochi
wametumia dakika moja kukaa kimya wakati wa kuanza kwa tukio hilo la
kuwakumbuka wahanga wa mashambulio Jijini Copenhagen.
Watu wawili wameuwawa na polisi
watano wamejeruhiwa katika mashambulio yaliyofanyika kwenye mdahalo
wa uhuru wa kuongea pamoja na kwenye hekalu. Mtu aliyehusika na tukio
hilo naye alipigwa risasi na kufa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni