Vikosi vya jeshi la Nigeria
vikisaidiwa na mashambulizi ya angani vimetwaa miji miwili ya Monguno
na Marte iliyokuwa ikishikiliwa na kundi la Boko Haram.
Wakati huo huo nchi ya Cameroon
imesema jeshi lake limewauwa zaidi ya wapiganaji 80 Boko Haram na
kuwakamata watu 1,000 wanaowaunga mkono.
Vile vile nchi Niger nayo jana
imesema imewakamata watu 160 wenye uhusiano na kundi la Boko Haram
tangu Februari 6, mwaka huu.
Nchi za Nigeria, Chad, Cameroon
pamoja na Niger hivi karibuni zimeunda ushirikiano wa kijeshi dhidi
ya kundi hilo la wapiganaji wa Kiislam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni