Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani
Papa Francis amelaani kuuwawa kwa kuchinjwa wakristo 21 wa dhehebu la
Coptic raia wa Misri, na wapiganaji wa kundi la dola ya Kiislam IS
nchini Libya, na kutangaza kuwa waliouwawa ni mashahidi wa imani na
kusema kuwa wakristo wote ni wamoja bila ya kujali madhehebu yao.
Papa amelazimika kutoa kauli yake
katika mkutano usio rasmi baada ya vyombo vya habari vya nchini Libya
kutoa taarifa za kutekwa Wamisri wengine 35 katika eneo moja la Libya
linaloshikiliwa na wapiganaji wa kundi la IS.
Utekaji nyara huo wa raia wengine wa
Misri umekuja baada ya Misri kujibu mapigo ya dola ya Kiislam IS kwa
kufanya mashambulizi ya anga katika kambi zao, ambapo mkuu wa jeshi
la nchi hiyo amesema watu 50 wameuwawa.
Wapiganaji wa IS wakijiandaa kuwachinja Wakristo 21 raia wa Misri
Bahari ya ikiwa imetapakaa damu ya watu 21 waliouwawa kikatili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni