Ujumbe wa Tanzania chini ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukionyesha namna Serikali ya Singapore inavyoratibu upatikanaji wa nyumba kwa wananchi wake ulipotembelea Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya Singapore jana.Jumla ya nyumba 900,000 zimeshajengwa na Bodi hii na kupatiwa wananchi kupitia ruzuku ya serikali na nyumba 50,000 zinapangishwa kwa wananchi kwa kodi isiyozidi asilimia 5. Taifa la Singapore lina watu milioni 5.4 na asilimia 99 ya watu wan chi hiyo wamewezeshwa kumiliki nyumba.
Ujumbe wa Tanzania ukitembelea vyumba vya mfano vya ukubwa tofauti vinavyojengwa na Bodi ya nyumba ya Singapore kwa ajili ya kuuzia au kupangisha wananchi kulingana na uwezo, mahitaji na ukubwa wa familia. Vyumba hivi vipo Makao Makuu ya Bodi ya Nyumba ya Singapore ambavyo ni kivutio kwa wageni wanaotembelea jengo hilo kujifunza namna ya kuhudumia watu wa kada mbalimbali wanaohitaji nyumba.
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa historia ya hatua mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nyumba nchini Singapore walipotembelea Bodi ya Maendeleo ya nyumba nchini humo jana.
Ujumbe wa Waziri Lukuvi ukiwa katika mji wa kisasa wa Punggol wenye ukubwa wa kilomita za mraba kumi ambao una nyumba zilizojengwa na Bodi ya Maendeleo ya Nyumba Singapore kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati na chini. Katika eneo hili nyumba zimewekewa miundombinu ya kisasa na zina watu wanaofikia 250,000. Hapa ni ghorofa ya pili ya jengo mojawapo lililojengwa katika mji huu wa kisasa.
Mojawapo wa majengo ya kisasa katika mji wa Punggol nchini Singapore yanayokaliwa na wananchi waliouziwa na Bodi ya Nyumba ya Singapore kupitia mifuko ya jamii na ruzuku ya serikali
Ujumbe wa Tanzania ukiwa eneo la Punggol Point Park ambalo ng’ambo yake ni bandari ya nchi ya Malaysia inayopakana kwa karibu na nchi ya Singapore.
Ujumbe wa Waziri William Vangimembe Lukuvi ukiingia Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore ulipotembelea Wizara hiyo jana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akiweka saini kwenye kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuingia Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angela Kairuki.
Mh. Waziri Lukuvi akisalimiana na Waziri wa Nchi Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Singapore Bw. Masagos alipotembelea Wizara hiyo jana.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi Mwandamizi Mambo ya Nje wa Singapore. Katika mazungumzo hayo Tanzania imeiomba Serikali ya Singapore kuwekeza nchini Tanzania hususan kwenye sekta ya nyumba, kusaidia upangaji wa miji mikubwa na kuanzisha safari za ndege kuja Tanzania ili kuvutia utalii. Nchi ya Singapore hupokea ndege 5800 kwa wiki kutoka nchi mbalimbali duniani na ina zaidi ya ndege 200 zinazoenda mataifa mbalimbali duniani hivyo kuwa kivutio kikubwa kuliko Tokyo Japan.
Waziri William Lukuvi akimpa zawadi ya kahawa na chai ya Tanzania, Waziri Mwandamizi wa Nchi ya Singapore Bw. Masagos kama ishara ya kutangaza bidhaa za Tanzania
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Singapore mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Wizara hiyo jana kuvutia ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Singapore.
Ujumbe wa Tanzania ukipata maelezo ya jinsi Shirika la Mipango Miji nchini Singapore la Surbana linavyokabiliana na uhaba wa ardhi katika nchi hiyo. Katika maelezo yake Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Bw. Pang Yee Ean alisema mipango ya ardhi ya Singapore huhuishwa kila baada ya miaka mitano ili iendane na hali ya uchumi na mahitaji na kuna nidhamu ya hali ya juu katika upangaji na matumizi ya ardhi ya nchi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni