Makoye alishinda kiti hicho katika
uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana,
akiwa ameongoza mtaa huo kwa awamu ya pili baada ya kuongoza miaka
mitano iliyopita.
Mke wa marehemu, Ivona Polikalapo,
amesema jana saa 10 jioni alimsikia mumewe akiongea na mtu kwenye
simu yake ya mkononi na kumsisitiza anahitaji mzigo wake wote.
Amesema ilipofika saa 10 alfajiri
leo, mbwa wao walisikika wakibweka kwa muda mrefu hali iliyomfanya
marehemu atoke nje kuangalia kilichopo katika banda lao la mifugo
huku (mke) akiendelea kuandaa chakula cha mifugo.
Mama huyo anasema baada ya muda
alitoka nje kwenda kumwaga uchafu shimoni, lakini alishangazwa
kumuona ananing’inia juu ya mti na alipojaribu kumuita hakuweza
kuitika.
Hata hivyo, kaimu kamanda wa polisi
mkoa wa Mwanza, Japhet Lusingu, amethibitisha kuwapo na tukio hilo na
kusema amejinyonga huku chanzo chake hakijafahamika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni