Nchi ya Malawi inatarajia kuridhia
sheria mpya inayopiga marufuku ndoa za watoto ambapo taifa hilo kwa
sasa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ndoa za watoto duniani.
Wabunge wa nchi hiyo ndogo ya kusini
mwa Afrika wiki iliyopita walipitisha muswada ambao unataongeza umri
wa kuoa kutoka umri wa miaka 16 hadi miaka 18.
Wanaharakati za haki za binadamu na
wabunge wanasema Malawi inandoa nyingi za watoto, ambapo watoto wa
kike wenye umri wa miaka 10 huozwa.
Chini ya Sheria za nchi hiyo rais
Peter Mutharika anamuda wa wiki tatu za kutia saini muswada huo wa
ndoa, talaka na mahusiano ya familia ili kuwa sheria baada ya
kuidhinishwa na wabunge kesho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni