Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa uzinduzi wa mchakato wa usajili wa vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (kulia).Mzee Augustino Mtauka akisaini fomu za usajili wa kituo kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati), usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu chaDar es Salaam (UDSM).
Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF-Real Madrid Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
Mtoto Osama Rashid akijaza fomu maalum kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Kulia ni mama yake Tatu Ali akishuhudia.
Baadhi ya wazazi wakiondoka katika uwanja wa Karume baada ya kuandikisha watoto wao.
Badhi ya wazazi wakiwasimamia watoto wao katika zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (wa pili kulia) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (kushoto) wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuandikisha vijana watakaojiunga na kituo kipya cha michezo.Baadhi ya wadau wa soka wakiwa wameleta watoto wao kujisajili katika zoezi hilo.
Vijana wakiingia katika uwanja wa Karume kwa ajili ya zoezi la kujisajili na hatimaye kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mwakilishi wa FIFA katika masuala ya michezo hapa nchini, Henry Tandau (katikati) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa zoezi la kandikisha vijana watakaojiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mtoto Issa Hashim akijaziwa fomu na Aisha Hashimu
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kushirikiana na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, limezindua mchakato wa usajili wa vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga na NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mchakato huo wa usajili umefanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambako watoto kutoka Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni walisajiliwa na kuruhusiwa, zoezi linalotarajia kuendelea leo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, aliwaka Watanzaia kuwaleta vijana wao katika mchakato huo, na kwamba hakutakuwa na urasimu utakaowakwamisha kusajiliwa.
Magori alisema kuwa, jukumu la kama NSSF ni kuratibu usajili wa vijana wasiopungua 500, ambao watafanyiwa mchujo na Real Madrid kupata nyota 30 ambao wataingia rasmi katika darasa la kwanza kabisa la akademi hiyo inayosubiriwa kwa hamu nchini.
“Wataalamu wanane wa lishe, tiba, afya na soka kutoka Madrid watatua nchini wiki ijayo, kuwafanyia mchujo vijana wapatao 500 tunaotarajia kuwasajili leo, kesho na wikiendi ijayo, ambao watafanya majaribio ya uwanjani Februari 28,” alisema Magori.
Aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye vipaji, kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwafikisha watoto wao kwenye usajili, ili kuwawezesha kupata nafasi ya kuwania kuingia miongoni mwa wakali 30 wa awali watakaofungua darasa la akademi hiyo.
Alibainisha kuwa, kutokana na uharaka wa uanzishwaji wa kituo, NSSF na Real Madrid hawatoweza kutembelea mikoani kufanya usajili kama huo mwaka huu, badala yake akawataka wazazi wanaoweza kufika na watoto wao Dar es Salaam kufanya hivyo.
Magori aliongeza kuwa, watoto watakaopata nafasi ya kuingia katika akademi yao watasoma na kujifunza soka, ambapo watakaozivutia timu mbalimbali barani Ulaya watauzwa na wale watakaokwama, watauzwa Afrika, ikiwamo kuunda timu ya NSSF.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni