Staa wa muziki Jaguar wa nchini
Kenya, ameamua kutumia kiasi cha shilingi milioni 1 na nusu za Kenya
kununua kipaza sauti cha dhahabu ambacho atakuwa akikitumia katika
maonyesho yake.
Jaguar ameamua kuchukua hatua hii
kama njia mojawapo ya kuonyesha namna ambavyo anaipenda na kuithamini
kazi yake, ambapo ameweka picha yake katika mtandao sambamba na
maneno yanayosomeka “Getting golden..I Love my job”.
Hatua hii ya Jaguar inakuwa ni
uthibitisho mwingine wa uwezo mkubwa alio nao kifedha kutokana na
uwekezaji ambao amekufanya katika muziki na pia biashara zake
binafsi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni