Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta
amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini
(TPA), Mhandisi Madeni Kipande kwa tuhuma za utendaji mbovu, ikiwa ni
pamoja na kutokuwepo kwa uwazi kwenye mamlaka hiyo hususani katika
michakato ya zabuni mbalimbali zinazotangazwa na mamlaka hiyo.
Pamoja na kuchukua uamuzi huo Mhe.
Sitta, ameunda tume ya watu sita itakayokuwa na jukumu la kuchunguza
tuhuma zinazomkabilia Mhandisi Kipande ambaye atakuwa nje ya madaraka
kwa muda wa wiki mbili kupisha uchunguzi huo na nafasi yake
itakaimiwa na Meneja wa Bandari Dar es Salaam Bw. Awadhi Masawe.
Mhandisi Madeni Kipande
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni