Mvutano baina ya serikali ya Kenya
na vituo vikuu vitatu vya televisheni unaingia siku ya tatu hii leo
huku idadi kubwa ya wananchi wakishindwa kuona matangazo ya
televisheni kwenye runinga zao kutokana na kuzimwa mitambo ya
analojia, siku ya jumamosi.
Waziri wa Teknolojia na Mawasiliano
Fred Matiang'i amevishutumu vyombo vya habari vya Standard Group,
Nation Media Group na Royal Media akivituhumu kujaribu kuishinikiza
serikali kwa kuzima mitambo yao wenyewe.
Hata hivyo taarifa hiyo imekosolewa
vikali na vyombo hivyo vitatu vinavyomiliki vituo vya NTV, QTV, KTN
na CITIZEN TV ambavyo wameishutumu serikali kwa kuhusika kuzima
mitambo yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni