Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi.
Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishirini na saba ( 27 ) zilizotokana na:-
a) Kufariki dunia kwa Wakuu wa Wilaya watatu ( 3 )
b) Kupandishwa cheo kwa Wakuu wa Wilaya 5 kuwa Wakuu wa Mikoa
C) Kupangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya 7, na
d) Kutengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 12.
Katika mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais amewateua Wakuu wapya wa Wilaya 27 ili kujaza nafasi hizo wazi.
Aidha, Wakuu wa Wilaya sitini na nne ( 64 ) wamebadilishwa vituo vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili ( 42 ) wameendelea kubaki katika vituo vya sasa.
1) Wakuu wa Wilaya waliofariki dunia
1.Capt. (MST ) James Yamungu - Serengeti
2.Anna J.Magoha - Urambo
3.Moshi M.Chang'a - Kalambo
TAARIFA KAMILI NI KAMA IFUATAVYO HAPO CHINI
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni