.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Februari 2015

VIJANA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI WAHAMASISHWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendleo ya Jamii Bw. Xavier Keebwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa vijana kuhusu Sera ya maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Ujuzi, Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambapo jumla ya zaidi ya Vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijini mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbvi wa manispaa hiyo. Kutoka Kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo kutoka wizara hiyo Bibi. Esther Riwa.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada wakati wa warsha biliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuhusu Mfuko wa maendeleo y Vijana nchini. Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo jumla ya zaidi ya vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa hiyo, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Peace Group kilichopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Bibi. Cecilia Alphonce walipotembelea kikundi hicho kwa ajili ya kukagua shughuli zao leo mkoani Kigoma.Kikundi hicho kinajishughulisha na uzalishaji wa miche ya miti na maua na kinaundwa na wanachama watano.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa miche ya maua kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha Peace Group kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji Bibi. Angelina G. Masunzu leo wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Vijana mkoani Kigoma.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akijaribu namna mashine ya kuchana mbao inavyofanya kazi walipotembelea Kikundi cha Vijana cha Ubhumwe Carpenter Cooperative cha mjini Kigoma leo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Gasto Yagaza.
Karani wa Kigoma Youth Entrepreneur Saccos Bibi.Fatuma Hamisi akisoma taarifa ya Saccos hiyo mbele ya Wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembela katika ofisi za Saccos hiyo leo mjini Kigoma. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Saccos hiyo Bw. Kapele Shaban, Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara hiyo Bibi. Esther Riwa na Katibu wa Saccos hiyo Bw. Ramadhan Daud.
Wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa (katikati) na Afisa Vijana wa Wizara hiyo Bibi. Amina Sanga (kushoto) wakiangalia nyaraka za usajili wa Saccos ya Kigoma Youth Entrepreneur Saccos iliyopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji leo. Kulia ni Katibu wa Saccos hiyo Bw. Ramadhan Daud. Picha na Frank Shija, WHVUM

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni