Watu 20 wamekufa kufuatia kutokea
milipuko kwenye eneo la ukaguzi la jeshi katika mji wa Biu
kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Vikosi vya jeshi katika eneo hilo
vilifyatua risasi na kuwauwa wapiganaji 17 ambao inaaminika kuwa ni
wa kundi la Boko Haram.
Siku ya jumanne kundi hilo la Boko
Haram lilitoa video ambayo kiongozi wao Abubakar Shekau alionekana
akiapa kuwa atavuruga uchaguzi usifanyike kwa gharama yotoye ile.
Video hiyo ya dakika 15 ilitolewa
kupitia akaunti yao ya twitta, jambo ambalo baadhi ya wachambuzi
wanahisi kundi hilo limeshawishika kuwa na akunti hiyo na kundi la
Dola ya Kiislam (IS).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni