Muigizaji filamu nyota nchini
Marekani Angelina Jolie amefanyiwa upasuaji wa kuondolewa shingo ya
uzazi pamoja na mirija ya uzazi, ili kumuepusha na saratani.
Katika maandiko aliyoyatoa kwenye
jarida la New York Times, Jolie amesema wiki iliyopita alifanya
vipimo na kubaini anaasilimia 50 ya uwezekano wa kupata saratani ya
shingo ya uzazi.
Miaka miwili iliyopita Jolie, ambaye
mama yake alifariki dunia kwa ugonjwa wa saratani, alifanyiwa
upasuaji mara mbili wa kuondoa sehemu ya nyama ya matiti kumuepusha
na saratani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni