Waziri Mkuu wa Yemeni, ametoa wito
kwa mataifa ya huba ya Kiarabu, kuingilia kati kuzuia waasi wa Shia
Houthi kufika kusini mwa nchi hiyo.
Waasi wa Houthis wamemng'oa rais
Abdrabbuh Mansour Hadi mwezi uliopita, ambaye amekimbilia eneo la
kusini mwa mji wa bandari wa Aden ambao umetambulishwa kama ngome ya
kuwadhibiti waasi.
Mwishoni mwa wiki waasi wa Houthis
waliutwaa mji wa Taiz, ambao ni watatu kwa ukubwa nchini Yemen, na
kuwafanya wakaribie mji wa Aden. Umoja wa Mataifa Yemen inaelekea
kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni