‘Model’ wa kiume, kike watia fora na mavazi ya ubunifu ‘run way’
yabamba ndani ya dakika
20.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Ile shoo maalum ya mwaka iliyokuwa
ikisubiriwa kwa hamu kubwa hatimaye usiku wa Machi 21 ndani ya Serena
Hotel jijini Dar es Salaam, shoo hiyo ‘Mercedes Benz Ally Remtullah 2015
Eleganza’ imeweza kuwa ya aina yake na ya kipekee kwa kuvutia kila
mmoja aliyehudhuria shoo hiyo.
Kama kawaida yake mbunifu wa mavazi, Ally
Remtullah amekuwa akifanya vizuri kila mwaka kwenye shoo zake hizo
anazoziandaa ambapo kwa shoo ya mwaka huu imezidi kuingia kwenye
historia kwa kuonyesha toleo jipya ‘New collection
2015’.
Miongoni mwa mambo yaliyoweza kubamba katika
shoo hiyo ni pamoja na jukwaa ‘Run way’ kwa Models hao kulitendea haki
na na kuonekana tukio la
Kimataifa.
Ni dhahiri shoo hiyo kwa kila aliyeshuhudia
asilimia 100, ni ya Kimataifa. Ambapo ilichukua ndani ya dakika 20 huku
kila Model akipangilia vilivyo na mavazi maalum hali iliyopelekea
kuliteka jukwaa.
Aidha, kwa upande wake Ally Remtullah
alipongeza wadau wote kwa kuendelea kumuunga mkono ambapo aliiambia Modewji
blog kuwa baada ya hapo anatarajia kuendelea kufanya
maonyesho zaidi ikiwemo ndani na nje ya
nchi.
Pia aliwashukuru wadhamini akiwemo mdhamini
Mkuu, Kampuni ya CFAO Motors LTD wauzaji wa magari kupitia brand yake ya
Mercedes Benz. Wengine ni MeTL Group kupitia bidhaa za ki-elekroniki
za LG na wengine wengi.
Fuatana na camera ya modewji blog
kwa picha za 'Cat walk' ndani ya hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
























Hakuna maoni :
Chapisha Maoni