Mama mmoja huko Detroit nchini
Marekani amekamatwa na polisi baada ya miili ya watoto wawili kukutwa
ikiwa kwenye jokofu nyumbani kwake.
Maafisa wa Mahakama waliokuwa
wakitekeleza amri ya kuhamishwa mama huyo hapo jana, walibaini miili
hiyo ya mtoto wa kiume wa miaka 11 na mtoto wa kike wa miaka 14.
Polisi wa Detroit hawakutaja jina la
mwanamke huyo lakini wamesema miili hiyo ilikuwa imevingirishwa
kwenye mfuko mmoja wa plastiki.
Watoto wengine wawili wa mwanamke
huyo wenye umri wa miaka 11 na 17, waliokutwa kwenye nyumba ya
jirani, wamechukuliwa na kuhifadhiwa mahala salama na serikali.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni