Wanafunzi 25 pamoja na wafanyakazi
wa Chuo Kikuu cha Strathmore nchini Kenya wamelazwa kwenye hospitali
kadhaa Jijini Nairobi baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na
sumu.
Wanafunzi hao ni sehemu ya wengine
300, wengi wao wakiwa ni wa mwaka wa mwisho waliokula chakula wakati
wa sherehe ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho siku ya Ijumaa.
Saa chache baada ya kula chakula
hicho wanafunzi wapatao 80 walienda kwenye Zahanati ya Chuo hicho cha
Strathmore kupatiwa matibabu huku wengine wakitibiwa kwenye hospitali
kadhaa nyingine.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni