Watoto wapatao 500 wenye umri wa
kuanzia miaka 11 na chini ya hapo hawajulikani walipo katika mji wa
Damasak nchini Nigeria uliokuwa umetwaliwa na wapiganaji wa Boko
Haram.
Mfanyabiashara wa mji huo wa
kaskazini mashariki mwa Nigeria ameliambia shirika la Reuters kuwa
wapiganaji wa Boko Haram waliwachukua watoto hao na kukimbia nao.
Vikosi vya Niger pamoja na Chad
vimeutwa mji wa Damasak mapema mwezi huu, na kumaliza miezi kadhaa ya
kukaliwa na wapiganaji hao wa Boko Haram.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni