Mbunge wa Kenya Gideon Mwiti,
anayekabiliwa na tuhuma za kumbaka mke wa mtu amehojiwa na polisi kwa
muda wa saa sita na kisha kuchukuliwa na gari na kupelekwa mahala
pasipojulikana.
Daktari wa mbunge huyo Mwangi
Muchiri, ambaye anadaiwa kumfanyia kwa nguvu vipimo vya Ukimwi
mwanamke huyo naye pia ameitwa kutoa maelezo yake mbele ya Bodi ya
Madaktari Kenya.
Mbunge Gideon Mwiti, wa jimbo la
Imenti ya Kati, aliitwa na kuhojiwa katika kituo cha polisi cha
Gigiri na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Daniel Kandie.
Daktari wa mbunge huyo Dk. Mwangi
Muchiri


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni