Ndege ya Shirika la Ndege la
Ujerumani la German-wingsaina aina ya Airbus A320 ikiwa na abiria 142
na wahudumu wa ndege sita imeanguka nchini Ufaransa kati ya eneo la
Barcelonnette na Digne.
Maafisa wa Mamlaka ya Usalama wa
Ndege nchini Ufaransa kwa kushirikiana na polisi imesema ndege hiyo
ilikuwa ikitokea Barcelona kwenda mji wa Dusseldorf nchini
Ujerumani. Ndege hiyo inamilikiwa na shirika mama la Lufthansa.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
amesema haijabainishwa jinsi ajali hiyo ilivyotokea lakini inapelekea
kufikiria kuwa hakuna mtu aliyenusurika kwenye ajali hiyo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni