Wakati msako wa kuwakamata waganga
wapiga ramli chonganishi ukiendelea nchi nzima hasa katika mikoa ya
kanda ziwa, jeshi la polisi nchini limepewa onyo toka kwa wanganga wa
jadi juu ya vifaa vinavyokamatwa wakati wa msako wao.
Jeshi hilo limepewa tahadhali ya
kukumbana na hatari yeyote baadaye ikiwa wataendelea kukamata vifaa
hivyo vikiwamo vibuyu, vitambaa vyeupe na vyeusi, ngao, mikuki pamoja
na shanga huku likitakiwa kurejesha mara moja baadhi ya vifaa hivyo
ambavyo vimekamatwa.
Katibu mwenezi wa chama cha waganga
wa tiba asili nchini, (Chawatiata), Steven Sebastian kutoka Mwanza,
akizungumza katika mkutano wa waganga wa jadi wilaya ya Bariadi mkoa
wa Simiyu, amesema kitendo cha kuchukua vibuyu vyao,
kutawafedhehesha.
Sebastiani akizungumza mbele ya
kamanda wa polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo, amesema kitendo
kinachofanywa na jeshi hilo cha kukamata vifaa hivyo, ni kitendo cha
hatari kwani kinaweza kusababisha hali ya migogoro mikubwa kati ya
jeshi la polisi na jamii.
Sebastian alieleza vibuyu, vitambaa
vyeupe, na vyekundu, shanga, ngao, pamoja na mikuki ni vifaa ambavyo
waganga hao walirithishwa na wazee wa zamani ambao alieleza vifaa
hivyo walivitumia katika kutafuta uhuru.
Akizungumzia hilo, kamanda wa polisi
Mkumbo amesema siyo kweli waganga wa jadi wanaonewa ama kusingiziwa
wanapiga ramli chonganishi, bali kutokana na uchunguzi wao
wamebainika kuwapo na hali hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni