Picha adimu za kiongozi wa Al Qaeda
marehemu Osama Bin Laden zimetolewa akiwa anaishi katika maeneo ya
milima ya Tora Bora kabla ya kutimuliwa kwa mashambulio ya anga
yaliyomfanya akimbie makazi hayo kufuatia shambulio la Septemba 11.
Picha hizo zimetolewa wakati wa kesi
ya kushirikiano na Al Qaeda inayosikilizwa Jijini New York Marekani,
inayomkabili Luteni Khaled al-Fawwaz aliyetumika kama njia ya
mawasiliano kwa taasisi ya kigaidi Jijini London katika miaka ya
1990.
Picha hizo zilipigwa na mwandishi wa
Palestina Abdel Barri Atwan, ambaye alikaribishwa kwenye maficho hayo
mwaka 1996 kama sehemu ya mpango wa Bin Laden kusambaza ujumbe wa
chuki dhidi ya nchi za magharibi.
Osama Bin Laden akiongea na mwandishi al-Suri
Osama Bin Laden akitabasamu
Hapa Osama akiwa ndani ya pango akiongea na mwanshishi al-Suri
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni