Mafuriko yanayotokana na mvua za
masika yameuwa watu 65, wakiwemo watoto 35 katika Jiji la Lobito
nchini Angola.
Shirika la habari la taifa la nchi
hiyo Angop limesema kina cha maji ya mafuriko kilifikia urefu wa mita
3 katika baadhi ya maeneo ya mji huo siku ya jumatano.
Nyumba nyingi zimeharibika, na timu
ya uaokoaji bado inaendelea kuwatafuta waathirika zaidi wa mafuriko.
Rais wa Angola Jose Eduardo Santos
ameziagiza serikali za mitaa kutoa misaada ya kibinadamu kwa
waathirika wa mafuriko hayo. Eneo kubwa la Angola linakabiliwa na
mvua kubwa tangu mwezi Januari.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni