Makumi ya waandamanaji wamerejea
tena mitaani katika jimbo la Ferguson, Missouri nchini Marekani siku
moja tu baada ya polisi wawili wajeruhiwe na waandamanaji.
Mamlaka za jimbo hilo zimeendelea
na msako mapema leo, wakati polisi wawili waliojeruhiwa kwa kupigwa
risasi wakiruhusiwa kutoka hospitali.
Maandamano ya jana yaliyokuwa
yakipinga vitendo vya ubaguzi wa rangi vinavyofanywa na jeshi la
polisi, yalianza kwa amani, lakini baadae yaligeuka kuwa ya mapambano
na polisi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni