Seneta wa chama cha Republican Ted
Cruz amethibitisha kuwa atagombea urais wa Marekani mwaka 2016, na
kuwa mwanachama wa kwanza wa Republican kutangaza nia.
Cruz mwenye umri wa miaka 44 kutoka
Texas anatarajiwa kutangaza mipango yake katika hotuba yake
atakayotoa leo katika Chuo Kikuu cha Liberty huko Virginia.
Katika video iliyotumwa kwenye
twitta Cruz amesikika akisema ni wakati wa kizazi kipya chenye
ujasiri wa kuifanya Marekani kuwa imara tena.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni