Naibu Rais wa Kenya William Ruto
amesema serikali ya Kenya italipa gharama zote za matibabu ya
muigizaji mkongwe wa vichekesho Mzee Ojwang'.
Muigizaji huyo ambaye jina lake
halisi ni Benson Wanjau, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la macho
kutoona vizuri pamoja na kisukari na siku ya jumatano alilazwa kwenye
Lions SightFirst Eye iliyopo Loresho.
Kwa mujibu wa madaktari wanaomtibu
Mzee Ojwang' anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa macho hii leo.
Naibu Rais wa Kenya, kupitia akuanti
yake ya twitta amesema serikali itamlipia matibabu Mzee Ojwang' na
kumtakia apone haraka.
Taarifa za kuugua muigizaji huyo wa
kundi la Vitimbi zilisambaa mitandaoni, huku mitandao ya jamii
ikianzisha kampeni ya kumlipia gharama za matibabu kwa kutumia
#OkoaMzeeOjwang.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni