Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini
imesema Korea Kaskazini imefyatua makombora saba ya kufyatuliwa
kutoka aridhini yaliyolenga kwenye bahari.
Tukio hilo limefanywa katika siku ya
mwisho ya zoezi la kijeshi la kila mwaka linaloendeshwa kwa
ushirikiano wa Marekani na Korea Kusini.
Msemaji wa Korea Kusini amesema
kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alikuwepo wakati wa urushwaji
wa makombora hayo hapo jana kwenye pwani ya mashariki.
Zoezi hilo la kijeshi ambalo
serikali ya Pyongnyang huliita maandalizi ya uvamizi, daima limekuwa
likichochea uhasana baina ya mataifa hayo mawili ya Korea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni