Wananchi wakiwa wanajaribu kuwaokoa manusura wa ajali hiyo baada ya basi dogo la abiria kutumbukia katika daraja eneo la Ilongoboto
Wananchi wakifika eneo la tukio tayari kutoa msaada baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Watu 18 wamefariki dunia papo hapo na mwingine mmoja amefariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya basi dogo la abiria kutumbukia darajani katika eneo la Ilongoboto, Kiwira wilayani Tukuyu mkoani Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Amelitaja gari hilo ni Toyota Hiace lenye namba za usajili T 290 ABU ambalo lilikuwa linataka Uyole kuelekea Kiwira.
Amesema karibu abiria wote waliokuwa katika gari hilo walikuwa ni wafanya biashara na walikuwa wanaelekea gulioni katika eneo la Kiwira. Majeruhi ni watatu ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
Dereva ni mmoja wa waliofariki dunia katika ajali hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni