.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 17 Aprili 2015

JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAPATIWA NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA ASKARI WA WILAYA YA KALIUA

Mkuu wa wilaya ya Kaliua Venance Mwamoto ( kulia ) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Suzan Kaganda wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kwenda kuzitazama nyumba walizokabidhiwa jeshi hilo la polisi.
Moja ya nyumba ambayo imekabidhiwa kwa jeshi la polisi wilayani Kaliua kwa ajili ya makazi ya askari.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora, ACP Suzan Kaganda akiwa na mkuu wa wilaya ya Kaliua Venance Mwamoto wakijadiliana jambo baada ya kumaliza kukagua nyumba zilizokabidhiwa kwa ajili ya askari polisi wilayani humo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora katika wilaya ya Kaliua limekabidhiwa nyumba takribani tano ambazo zina uwezo wa kukaliwa na familia kumi na nne. 


Nyumba hizo zimekabidhiwa leo wakati Kamanda wa Polisi mkoa Tabora ACP Suzan Kaganda mapema leo tarhe 17.04.2014 alipotembelea wilaya ya Kaliua kujionea nyumba hizo, amabapo alisema amefarijika sana na kumpongeza Mkuu wa wilaya mpya wa willaya hiyo Mh. Venance Mwamoto kugundua changamoto zinazoikabli jeshi la Polisi hasa za makazi ya askari na pia kuishukuru H/mashauri ya (W) Kaliua kwa mchango wao.
 

Mkuu wa wilaya ya Kaliua kwa upande wake amesema kwamba toka aripoti aliziona changamoto hizo na hivyo akachukua maamuzi ya kuwapatia Jeshi la polisi wilaya ya Kaliua nyumba hizo ambazo ni mali ya shirika ya reli zilizokuwa zimetelekezwa bila kukaliwa na watu kwa takribani miaka 18, pia amesema atashirikiana na jeshi la Polisi na Halmashauri ya wilaya katika ukarabati wa nyumba hizo.


Jambo kubwa lililomsukumba kuwagaia nyumba hizo jeshi la Polisi ni changamoto ya makazi kwa askari, nyumba hizo kwa kukosa wakaaji zilikuwa zikitumika kama magenge ya uhalifu, na pia kuwepo kwa askari katika eneo moja.

Na. Fakih A. Mapondela - A/INSP Mkuu wa kitengo cha habari Polisi Tabora.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni