Michuano ya soka kwa ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam inaanza kutimua vumbi jumapili hii ya April 19/2015,kwa vilabu mbalimbali kuchuana vikali kuuwania ubingwa huo.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,maandalizi kuelekea michuano hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na viongozi wa vilabu husika kupewa kanuni na taratibu zitakazotumika katika mashindano.
Jumla ya vilabu vinane (8) vitashiriki katika ligi hiyo ya wanawake,ambavyo ni SIMBA QUEENS,REAL TANZANITE,TEMEKE SQUAD,EVER-GREEN QUEENS,JKT QUEENS,LULU QUEENS,MBURAHATI QUEENS na UZURI QUEENS.
Mechi ya ufunguzi itazikutanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens,itakayopigwa katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Kinondoni jijini Dar es salaam Jumapili ya April 19.
IMETOLEWA NA CHAMA CHA SOKA MKOA WA DAR ES SALAAM,DRFA
Omary Katanga,Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano,DRFA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni