Mwanamuziki Chris Brown akiwa ameshika chupa ya Shampeni huku pembeni wasichana warembo wakiwa wamebeba keki wakati wa sherehe yake ya kutimiza miaka 26 ya kuzaliwa kwake iliyofanyika katika kalbu ya Drai's mjini Las Vegas nchini Marekani.
Kati ya mastaa waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na bondia Floyd Mayweather ambaye alionyesha jeuri ya pesa.
Mayweather ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alimpiga mpinzani wake Manny Pacquiao katika ukumbi wa MGM Grande Arena, alionekana akitoa fedha " dola " katika begi maalum lililokuwa limebebwa na mmoja wa wapambe wake alioongozana nao katika sherehe hiyo.
Floyd Mayweather akitoa hela katika begi tayari kwa matumizi.
Mnakiona kibunda cha dola mia mia!! Mayweather akiwa ameshika kibunda cha dola mia mia tayari kulipa bili yake wakati wa sherehe ya miaka 26 ya mwanamuziki Chris Brown.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni