BONDIA Fransic Cheka atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kutoka jela ambapo atacheza na Kiatchai Singwancha kutoka Thailand mpambano huo wa raundi kumi utafanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam,
Akizungumza matayarisho ya mpambano huo, promota Kaike Siraju amesema kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa hivi sasa ambapo mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa wiki hii.
Mpambano huo utasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya rais wake Emanuel Mlundwa.
w
Wamesema kuwa wao wako tayali kwa mpambano huo, na bondia wa Thailand ataingia nchini siku tatu kabla ya mpambano huo ambao utavuta hisia za wapenzi wengi wa mchezo wa ndondi nchini. Sikuh iyo Vicent Mbilinyi 'Sugu' atavaana na Keis Amal.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakavyokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni