Mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid wamejiweka pabaya kusonga mbele kuelekea hatua ya fainali ya michuano hiyo, baada ya usiku wa kuamkia leo kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Kibibi kizee cha Turin, Juventus ya Italia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo.
Wakicheza ugenini, Real Madrid walijikuta wakifungwa bao la kwanza katika dakika ya nane ya mchezo, bao likifungwa na Alvaro Morata.
Hata hivyo mshambuliaji mwenye kasi na bidii uwanjani, Cristiano Ronaldo aliisawazishia timu yake ya Real Madrid kwa kichwa katika dakika ya 27 kwa kufunga bao safi, na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na walikuwa ni Juventus waliopata bao la pili kwa mkwaju wa penati iliyofungwa na mkongwe Carlos Tevez. Timu hizo zitarudiana wiki ijayo mjini Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Hadi mwisho wa mchezo huo, Juventus 2 na Real Madrid 1.
Ronaldo akifunga bao kwa kichwa
Maelfu ya mashabiki wakiwa wamefurika uwanjani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni