Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga akimkaribisha Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges (kulia) kuzungumza na wakunga nchini waliokusanyika kwenye mdahalo wa siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara. Kushoto ni Kaimu Muuguzi mkuu wa serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala. (Picha zote na Zainul Mzige)
Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges akizungumza na Wakunga nchini Tanzania waliohudhuria kwenye mdahalo wa siku moja uliofanyika kwenye ukumbi wa Mara ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mara mjini Musoma kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani kujadili changamoto zinazowakabili Wakunga nchini. Katikati ni Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga na Kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikalim kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges akisisitiza jambo wakati akiteta na Wakunga nchini ambapo pia aliwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka kuendeleza moyo huo bila kuchoka.
Daktari bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, Kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya mdahalo wa wakunga ambapo alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na huduma hafifu.
Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Felista Bwana akitoa mada kwenye mdahalo huo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga nchini waliohudhuria mdahalo huo wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mdahalo huo.
Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akielezea umuhimu wa Wakunga nchini kujiunga na chama hicho pamoja na faida watakazozipata pindi wawapo wanachama wa TAMA wakati wa mdahalo wa siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani mjini Musoma.
Kutoka kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Christine Kwayu, Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges pamoja na Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Felista Bwana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Lena Mfalila (kulia) akijumuika na Wakunga kuimba wimbo wa mshikamano na hamasa mara baada ya kusikiliza risala fupi ya Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges (hayupo pichani).
Baadhi ya Wakunda kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki kwenye mdahalo huo wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano.
Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Felista Bwana (kushoto) akishiriki kuimba wimbo huo wa mshikamano.
Na Mwandishi wetu, Musoma
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances
Ganges, ametoa wito wa wakunga na wauguzi kubadilisha uzoefu wa shughuli
zao ili kuhakikisha taifa linaondokana na vifo vya wanawake wajawazito
na watoto.
Akizungumza katika mdahalo kuelekea sherehe za kilele
cha maadhimisho ya siku ya wakunga duniani, iliyofanyika kitaifa mkoani
Mara, Ganges alisema kwamba ni wajibu wa wakunga kuhakikisha kwamba
dunia ya kesho inakuwa bora na wanaweza kwa kushirikiana na
kubadilishana uzoefu.
Alisema dunia inawategemea wauguzi
kuendeleza kizazi cha binadamu na katika kufanya hivyo kuna changamoto
nyingi zinazotokea changamoto ambazo zinaweza kumalizwa kwa kila mmoja
kutimiza wajibu wake katika eneo analofanyia kazi.
Aliutaja wajibu huo kama uongozi, uelimishaji na pia utendaji wa kazi wenye tija na busara.
Alisema nia ya siku ya wakunga ipo wazi ni kuleta ushirikiano kwa ajili ya kuleta dunia iliyo njema ya kesho.
Mtendaji
huyo wa Shirikisho hilo lenye makao makuu yake nchini Uholanzi alisema
kwamba wanafuraha kubwa kusikia mambo makubwa yanayofanywa na wakunga
nchini Tanzania pamoja na changamoto zake zilizopo.
Alisema mafanikio yaliyopo ni matokeo ya ushirikiano na ufanyaji kazi wa pamoja.Alisema
katika hotuba yake hiyo kwamba wakunga wana wajibu mkubwa wa
kuhakikisha watoto wanazaliwa salama, wanawake wanakuwa salama na kizazi
cha binadamu kinakuwa salama.
Wakati huo huo Programme
Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya
watu (UNFPA) Felista Bwana amesema tafiti zilizopo zinaonesha kuwepo na
idadi ndogo ya wakunga wataalamu na kwamba juhudi lazima zifanyike
kuhakikisha kwamba vituo vya afya vyote vina wakunga wataalamu.
Aidha
mratibu wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy alisema chama
hicho chenye wanachama 3000 miongoni mwa wakunga wauguzi elfu 39
kimelenga kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa anapata
huduma za mkunga mtaalamu .
Alisema kwa sasa ni asilimia 51 tu ya wanawake wazazi wanapata huduma ya wakunga wataalamu.
Alisema ipo haja ya kukubaliana kuwekeza kwa wakunga kwa ajili ya taifa la kesho.
Naye
Daktari bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya wakunga
alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na huduma hafifu.
Aliwataka
wakunga kutumia maarifa zaidi kuokoa maisha ya watoto na wazazi kwa
kuwa na maamuzi ya haraka yanayozingatia uwezo wa eneo analofanyia kazi
na kuhakikisha, kazi zisizowezekana zinapelekwa katika hatua afiki.
Alisema
ipo haja ya mara kwa mara kwa wakunga kuangalia mabadiliko mbalimbali
ya kazi zao kwa kufuatilia wenzao wamefanya nini na sasa tatizo
analoshughulikia wengine wamelifanyaje.
Alisisitiza haja ya ufanyaji maamuzi mapema ili kuokoa maisha ya mtoto na mzazi.
Alisema
hali hiyo inatokana na ukweli kuwa wazazi wenye uzazi pingamizi
hucheleweshewa kufanyiwa maamuzi na hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto na
mzazi.
Wakati huo huo Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA),
Feddy Mwanga alisema ipo haja ya wakunga kujitathmini na kushirikiana
ili kuhakikisha kwamba huduma wanayoitoa ni ya kiwango cha juu,
inayokubalika na kuvutia.
Alisema wanawake wanapoamua kuzalia kwa
wakunga wa kienyeji kuna haja ya kujiuliza kwanini wanafanya maamuzi
hayo wakati vituo vipo na wakunga wapo.
Alitaka wakunga
kufanyakazi zao kwa bidii na maarifa na kuhakikisha kwamba huduma zao
zinakubalika ili wazazi watumnie huduma zao na hivyo kuwezesha kuwa na
taifa bora.
Aidha alitaka watumie takwimu vyema katika kuboresha
huduma za ukunga katika maeneo yao na hasa kuhakikisha kwamba
zinafikika na zinafanyiwa kazi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni