.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Mei 2015

LIGI YA MABINGWA ULAYA, LIONEL MESSI APIGA MBILI NDANI YA DAKIKA TATU WAKATI FC BARCELONA WAKIITANDIKA BAYERN MUNICH 3-0 CAMP NOU


Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp, FC Barcelona wamewatandika wageni wao Bayern Munich jumla ya mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo. 

Barcelona wakicheza soka lao la kugongeana pasi za uhakika, walijipatia mabao yao kupitia kwa Lionel Messi ambaye alifunga mabao 2 katika dakika za 77 na 80 na bao la tatu likiwekwa kimiani na Neymar. 

Timu hizo zitarudiana wiki ijayo katika uwanja wa Allinz Arena. Bayern ili wafuzu kwa hatua ya fainali, itabidi wawafunge Barcelona si chini ya mabao 4-0, vinginevyo safari ndiyo inaenda kukamilishwa nyumbani kwao.
DUH WAMENIDHALILISHA!! Kocha mkuu wa Bayern Munich, Pep Guardiola akitoka uwanjani kichwa chini baada ya kushuhudia timu yake ikichapwa mabao 3-0 na FC Barcelona. Guardiola kabla ya kutimkia Bayern, alikuwa kocha wa FC Barcelona.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni