Mahakama nchini India imemtia
hatiani muigizaji nyota wa Bollywood, Salman Khan kwa kumuua mtu
asiye na makazi katika tukio la mwaka 2002 la kugonga watu kwa gari
na kisha kukimbia Mjini Mumbai.
Mtu huyo mwanaume aliyekufa ni
miongoni mwa watu watano waliogongwa kwa gari, ambapo muigizaji huyo
alifunguliwa mashtaka ya mauaji.
Katika utetezi wake Khan amesema
dereva wake alikuwa ndie anaendesha gari, lakini Jaji amesema
muigizaji huyo ndiye aliyekuwa anaendesha gari huku akiwa amelewa.
Hukumu bado haijatajwa na anakabiliwa na kifungo kisichozidi miaka
10.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni