Kivuko kinatarajiwa kuanza kufanya
shughuli ya kuvusha watu kutoka Florida kwenda Cuba, kwa mara ya
kwanza tangu miaka 50 kupita baada ya serikali ya Marekani kuridhia
huduma hiyo mpya ya usafiri.
Huduma za kivuko hicho zilisitishwa
baini ya mataifa hayo majirani, baada ya Marekani kuiwekea vikwazo
vya kiuchumi Cuba mnamo mwaka 1960.
Hata hivyo Marekani ilitangaza
kurejesha mahusiano ya kidiplomasia mwezi Desemba mwaka jana, kwa
kuondoa vikwazo na idadi kadhaa za vivuko zimepewa leseni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni