Wanafamilia wa Bobbi Kristina Brown
wamekusanyika huku kukiwa na hofu kwamba anaelekea kushindwa
kupigania uhai wake kwa karibu miezi mitano tangu akutwe hoi bafuni.
Shangazi yake Pat Houston ameonekana
akiwakumbatia marafiki na ndugu wakati alipotembelea chumba cha
wagonjwa mahututi chini ya uangalizi kwa saa 24 ambapo Bobbi
Kristina, amelazwa.
Kitendo cha kuwasili kwa gari la
kubebea maiti na kuwekwa kwa turubai kumeibua hisia huenda hali ya
Bobbi Kristina ni mbaya mno.
Maafisa wa polisi wawili jana usiku
walifika hospitali, lakini hadi sasa uvumi unaendelea iwapo rafiki wa
kiume wa Bobbi Kristina atafunguliwa mashtaka kwa kuhusika na gali
yake.
Wanafamilia ya Bobbi Kristina wakitoka kumuangalia
Gari la kubebea jeneza pamoja na hema likioneka
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni