.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Julai 2015

KAMISHNA MKUU WA MAONESHO YA EXPO MILAN 2015 AIPONGEZA TANZANIA KWA KUWAVUTIA WAWEKEZAJI TOKA NJE


                                                                                          Na: Khamis Haji, Italy
 

Waandaaji wa maonesho ya biashara ya kimataifa nchini Italia wamesema matarajio yao ni Tanzania kupokea wawekezaji wengi wa vitega uchumi na wafanyabiashara wakubwa baada ya kuzitangaza kikamilifu na rasilimali ilizonazo katika maonesho hayo.
 

Kamishna Mkuu wa maonesho ya Expo Milan 2015, Bruno Pasquino amesema hatua hiyo ya Tanzania itawapa ufahamu mkubwa wawekezaji, wafanyabiashara na watu kutoka mataifa tafauti wanaofika katika maoneshi hayo na baadaye wataona maeneo wanayohitaji kuwekeza.
 

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Tanzania katika maonesho hayo amesema wawekezaji wengi wanavutiwa na sekta ya utalii na kilimo ikiwemo cha viungo maeneo ambayo Tanzania imejipanga vizuri kuonesha uliomo katika sekta hizo.
 

“Italia hata kabla ya maonesho haya tumekuwa na mahusiano mazuri katika biashara na uwekezaji, bila shaka hatua yenu ya kushiriki na kujitangaza kikamilifu yatawapa uelewa zaidi washiriki na baadaye kuona maeneo yanayowafaa”, alisema Kamishna huyo.
 

Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika maonesho hayo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema juhudi kubwa zimechukuliwa na Tanzania Bara na Zanzibar kuweka mazingira mazuri bora kwa wawekezaji vitegauchumi.
 

Alisema ushuriki wa Tanzania katika maonesho hayo mbali na kujitangaza yenyewe, pia utaipa nafasi kuona maeneo mbali mbali nchin Itali na nchi nyengine washiriki ambazo inaweza kushirikiano nazo kwa azma ya kupanua biashara na uwekezaji.
 

Maalim Seif alisema zipo fursa nyingi Tanzania ambazo wawekezaji wanaweza kufungua miradi yao, zikiwemo mazao ya viungo, kama vile karafuu, madini ya aina tafautii, na sekta ya utalii ambayo imekuwa na fursa ya kipekee kutokana na vivutio vingi vilivyopo.

 

Alisema baadhi ya vivutio hivyo ni mlima Kilimanjaro, maeneo ya kihistoria ukiwemo Mji Mkongwe wa Zanzibar, mbuga za wanyama, pamoja na fukwe za bahari zenye mandhari mazuri yenye kuvutia. 

Katika maonesho hayo, Maalim Seif ambaye amefuatana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui na Balozi wa Tanzania, James Msekela alitembelea mabanda ya nchi mbali mbali, ikiwemo Italia, Kazakhstan na mabanda ya nchi za Afrika Mashariki, ambazo ni Uganda, Burundi, Kenya na Rwanda.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni