Ziara ya rais Barack Obama nchini
Kenya imekutana na kuibuka kwa habari kuwa wakala wa serikali ya
Kenya bado unashikilia fedha zilizoachwa na baba wa rais huyo wa
Marekani ambaye alifariki dunia mwaka 1982.
Wakati Rais Obama akitarajiwa kuwapo
Kenya wiki ijayo, Mamlaka ya Fedha za Madai zisizo na Mdai (UFAA)
inashikilia shilingi 53,933 zinazopaswa kuchukuliwa na familia ya
marehemu Barack Hussein Obama.
Baba wa rais Obama alifariki dunia
katika ajali ya gari na fedha kutoka kwa bima yake ya maisha ambayo
aliikata haijadaiwa na warithi wake hadi sasa, Mwenyekiti wa UFAA,
Vincent Kimosop ameeleza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni